Kama vile kila mtu
ana alama za vidole za kipekee, kila mtu pia ana ubongo
wa kipekee. Ni huu upekee unaotufanya wale tulio.
Chukulia kwa mfano upekee wa ubongo wako ulifanya tiba
kwa ugonjwa wa binadamu ulioogofiwa, Je, itakuwa jukumu
lako kwa binadamu wenzako kudhihirisha tiba hiyo?
Utashiriki kipande hicho cha upekee wako na wengine?
Lakini inafaa hivyo ikiwa wapania kupunguza usumbufu!
Wakati unafichua udhalimu unaofanyiwa binadamu wenzako
ni wajibu wako kudhihirisha udhalimu huo? Musa alihisi
inamfaa, Jefferson alijua inamfaa, Ghadi alidhamiri
inamfaa, Joan wa Are kwa ukweli aliamua inamfaa.
Tunapoona wanadamu wakipungua tuna jukumu la kufaamisha
ulimwengu mabaya haya.
Hata hivyo kuna tofauti kubwa kati ya kudhihirisha tiba
kwa ugonjwa na kudhihirisha makosa yaliyopatikana kuwa
ukweli. Kufanya ijulikane ya kwanza ni uchangamfu,
kufanya ijulikane ya pili huhitaji ushupavu kwa wale
watu mashuli yaliyoendelea kwa kupunga wengine hukereka
kuona mapato yao yakikatizwa. Kwa hivyo ilivyokuwa siku
za utumwa katika karne ya kumi na tisa; ndivyo ilivyo
hata karne hii ya ishirini na moja! Ndivyo itakavyokuwa
wakati ghadhabu inayotarajiwa, ya wapokezi fulani wa
zaka watakaposoma kijitabu hiki na kumtusi mwandishi
wake kuwa mwongo, mtovu wa nidhamu na hulka njema na
mtaja jina la Mungu kwa uwongo.
Lakini kunaweza kuwa wahubiri fulani wasio na habari
wapokeao zaka wasiojua mafundisho ya Biblia kuhusu
maudhui ya zaka na usaidizi wa kanisa, lakini baada ya
kusoma somo hili hata hawa wasio na habari hawataweza
kujitetea kwa kutojua. Hata hivyo ni mkuu wetu aliyesema
“Wamebarikiwa wakati binadamu watawatusi na kuwadhulumu
na kusema kila aina ya uwongo kuwahusu, kwa jina langu.
Furahi kwani ni mkuu ujira wenu mbinguni ilinyokuwa kwa
watabiri walioishi mbele yenu (Matayo 5:11,12).
Somo hili linawalenga wakristo wote wanaohitaji kujua
mafundisho ya Biblia kuhusu zaka.
ZAKA: BIASHARA KUU .
(Ulaji wa kikanisa au uhitaji wa binadamu?)
Zaka ni chanzo cha mapato kwa mashirika mengi ya
makanisa ya kikristo. Katika mashirika ya pwani
ilichapisha mapato ya zaka ya mwaka. Kongamano hili
lenye wat takribani 22,500 liliripoti mapato yake ya
zaka ya takribani pauni 18,000. Haya ni kama pauni 800
kwa kila mtu. Lakini kumbuka hii haijumuishi matoleo
wanachama waliopeana kwa makanisa yao na kongamano kwa
kuongezeka kwa zaka.
Nikiwa nimekaa katika kamati mbili za makongamano ya
kikristo kwa jumla ya miaka kumi na mitan, ninaweza
kusema kwa ukweli kwa maoni yangu, kila moja la
mashirika haya lilipata fanaka kutokana na zaka na
wanachama, yalioangaziwa kila mara.
Jambo la tatu lilioangaziwa lilikuwa kuongezeka kwa
mtaji, ujenzi wa makanisa kwa uzingatifu. Kanisa
lilianzisha mfuko maalum wa kukopa makanisa pesa za
kujengea majengo mapya na kukarabati yale yaliyochakaa.
Lakini katika hili kanisa hata kama wanakanisa hulipia
ardhi na jengo, shirika la conference, si wanakanisa
wanaolipa madeni, huwa na hati ya umilki mali yote ya
kanisa.
Wakati wa huduma hii ya kujitolea katika kamati zote
mbili siwezi kukumbuka kamati yoyote ya conference
ikizungumzia vile itakavyosaidia wajane, wakiwa na
maskwota katika mipaka yake. Mkazo mkubwa ulitiliwa
uendeshaji wa hospitali hata hivyo.
Pengine sababu kubwa isiyosemwa kwa kutilia maanani
hospitali na kupuuza makao ya yatima, wajane na maskwota
ni kwa kuwa hospitali huleta faida ilhali haya mengine
yanadhaniwa kupunguza pesa za kanisa.
Unauliza (kwa nini hukusema wakati huo?) Wacha
niwahakikishie kuwa wakati huo sikujua vizuri juu ya
mafundisho ya kanisa lilikuwa linanifundisha injili ya
Biblia. Hata hivyo nilipoujua ukweli mwenyewe kupitia
kwa kusoma Biblia maombi na utafiti, sasa ninajaribu
kurekebisha makosa yangu ya miaka iliyotangulia.
Tusaidie ulaji huu wa kikanisa au mahitaji ya kibinadamu?
Yalioyangaziwa
Utatifiti huu uta: (1) Leta mafundisho ya Bibilia kuhusu
zaka, haja na kazi yake. (2) Onyesho kuwa kanisa yeyote
ya kikristo itumiayo zaka kama uchumi wqke inatakikana
kuwasilisha mpango huu kama jaribio la kibiashara ya
kikristo, sio kupitia kwa neno la Mungu.
Tafadhali kumbuka kuwa kando na historia husika
mwandishi huyu hutumia vianzao vya Biblia. kiwango cha
imani ya mkristo lazima kiwe maandiko sheria na ushuhuda
wala sio Papa Mtabiri, Mkuani, Mfalme, kamati.
Kitabu cha kanisa, utamaduni au chanzo chochote cha
kibinadamu kwa kuwa “……………. Kama wanazungumza sio
kulingana na neno hili, ni kwa sababu mwangaza ndani yao
(Isayo 8:20).
Ikiwa tu imetajwa, vifungo vyote vya Biblia
vilivyotumika hapa ni kutoa kwa Biblia ya Mfalme Yakobo.
SURA YA KWANZA
KUTOA ZAKA KATIKA AGANO LA KALE
Kulingana na (Walawi 27:32) zaka ni fungu la kumi la
faida ya mtu. Katika (kumbukumbu la torati 14:28)
Waisraeli waliambiwa walete zaka ya “nyongeza”.
Ni muhimu kukumbuka kuwa kutoa zaka kulikuwepo tangu
kabla historia ya Israeli.
Katika sherehe za wasemite na indo-German waliokuwa
hawamjui Mungu. Iliaminika kuwa kama miungu haingepokea
haki yao hawangepeana baraka zao mwaka uliofuata James
Hasstings, Kamusi ya Biblia 1005.
Pia, zaka haikuwa kawaida ikikusanywa kwa ajili kutoa
zaka kulikuwa miongoni mwa watu wa zamani “Kwa sababu
zao na zisizo za kikanisa…..” Kamusi ya Biblia ya
Seventh-Day Adventist, 1127.
Zaka, ikihitajika chini ya amri ya Musa.
Ukisoma zaka yote ilivyowashilishwa katika Biblia,
utagundua kuwa kutoa zaka kumetajwa kwa mara ya kwanza
katika (Mwanzo 14:17-24). Pale Abraham anapozungumziwa
“anayetoa” toleo la fungu la kumi kwa Melchizedek,
Mfalme wa salami.Walakini “tunalipa”, wajibu, lakini “tunatoa”,
zawadi kwa hiari. Hapakuwa na sheria ya kutoa zaka
katika neno la Mungu akimtaka Abraham amlipe Melchizedek
zaka kutokana na madhara ya vita.
Ni wazi, kutoa zaka kulijumulishwa katika amri ya Musa,
pamoja na matoleo ya kuchoma, kafara, ahadi na upashaji
tohara.
(Kumbukumbu la torati sura 11, 12, 14 na 26 Walawi sura
12) “Chini ya mfumo wa Walawi, Mungu akidhanisha …………..
Zaka ………….” Kamusi ya Biblia S.D.A, 1127.
Kwa sababu Abraham “alitoa” zaka kwa Melchizedek kabla
ya Musa na sheria za siku zake, baadhi ya kawaida.
Kuongezea baadhi ya makanisa hudadili kuwa Abraham
alimlipa vile maandishi yasemavyo sufiri nukta moja ya
uharibifu wa kivita wala sio moja juu ya kumi. Walawi
walipata moja juu ya hamsini ya uharibifu wa kivita wal
sio moja juu ya kumi. Sheria iliyohusu uharibifu wa
kivita haikuhusikana na zaka (Hesabu 31:27-28) sasa Musa
katika mwanzo alikuwa anaandikisha sheria ya jumla ya
kutoa zaka wakati wa Abraham. Kwa nini ajiondoe kwa
sheria hii miaka mia nne baadaye? Zawadi ya Abraham
ilikuwa ya kujitolea, toleo la shukrani bila nyogeza wa
upungufu.
Ni kweli kuwa kutoa zaka ilikuwa sehemu ya sheria
zilizoandikwa (kumbukumbu 14:22-29 na 26:12) lakini
wafalisayo wakauchukulia kuwa kulikuwa ni sheria ya
kawaida ya kutoa zaka wakati wa Abraham hufuatwa mara tu
baada ya mtu kupashwa tohara. Kutahiriwa kulikuwepo
kabla ya Musa (Mwanzo 17:10) na kulijumlishwa katika
sheria zingine kama kutoa zaka. (Walawi 12:3) Hata hivyo
tunavyoona katika wakolosai 2 – 16, Paulo anasema kuwa
kifo cha Yesu kilimaliza sheria za Musa (Waibrania 9:8 -
11) ikijumuisha tohara wagalatia 5:6 kwa hivyo hata kama
tohara na zaka vilikuwepo kabla ya Musa na kuandikwa kwa
sheria zake, hili halikufanya matendo haya kawaida.
LENGO NA MATUMIZI YA ZAKA
Kumbukumbu 14 Waziwazi na inatoa lengo la zaka na vile
ilivyotumika. Nukuu za vifungu 22 – 29 inaonyesha hivi.
Fungu 22 – Waisiraeli waliagaziwa kutoa zaka kwa
nyongeza ya mazao yao kila mwaka.
Fungu 23 – Mkulima na familia yake walikuwa watumie zaka
katika sherehe na katika kumheshimu Mungu aliyebariki
bidii yao katika mwaka uliotangulia na aliyependekeza
mahali pa dhabihu, walikuwa watoe mafuta, mzabibu na
wanyama.
Fungu 24 – 26 ikiwa mahali pa kutolewa dhabihu palikuwa
mbali basi mkulima na familia yake aliusa na kutoa zaka?
Yawezekana kuwa hajawahi haja yake kwa kuogopa uwongo
wake. Je? Wanaogopa kulewa kwenu jinsi Mungu alivyoagiza
zaka itumike wakati wa walawi?
Fungu 27 – Waliolinda madhabahu walihudumu kama wahubiri
walikuwa wapokee baadhi ya zaka sio kiwango fulani kwani
hawakuwa wamiliki mali, ardhi ingawa baadaye tukisoma
maagizo ya Paulo katika agano jipya kuhusu wahubiri
tutaona kuwa mfumo wa wahubiri wa siku ya Musa
ulifutiliwa mbali wakati yesu alipokuwa mhuburi mkuu wa
wote walioamini. Kwa hivyo mhubiri wako hachukui nafasi
ya mhubiri wa walawi, aliyechinjiwa kafara na akawa
mpatanishi kati ya mtenda dhambi na Mungu. Vile
tutakavyoona Paulo anafundisha kuwa kifo cha Yesu
kilichukua mahali pa kafara ya wanyama na Yesu pekee
ndiye aliyehudumu kama mpatanishi wa binadamu na Mungu.
Katika Matayo 25, tutaona Yesu pia akituambia tutakavyo
mpatia mhubiri wetu mkuu na jinsi ya kumtumikia, binafsi.
Fungu 28 – Katika mwisho wa mwaka wa tatu wa mfuatano
was sabato Waisraeli walikuwa walete zaka ya nyongeza na
walihifadhi katika hifadhi zao.
Fungu 29 – Tena walikuwa wapate sehemu ya zaka hili
zilikuwa zigharamie mahitaji ya wakimbizi, wajane na
yatima, walioishi vijijini mwa watoa zaka.
Fananisha fundisho hili la Biblia na lile la Ellen White
aliyeandika. Mmoja hufikiria kuwa zaka inaweza kutumika
katika kazi za shule. Na wengine hufikiria kuwa
watahitaji uungwaji mkono watakikana kusaidiwa na zaka.
Lakini kosa kubwa hutendwa wakati zaka haitumiki kwa
lengo la kuwasaidia wahuburi upigiaji mstari ni wangu
ushuda chapisho la 9,248 – 249.
Pia alifundisha kuwa zaka isitumike kuwasaidia (counses
of stewardship 103) kwa nini Bi. White haungi mafundisho
ya Biblia, kutumia zaka kuwasidia.
Baadhi ya watu wamesema kuwa kumbukumbu la torati 14
inazungumzia zaka ya pili, sio ya pili kusoma hili, mtu
ajifikiriaye vizuri hulipata ombo. Kwanza hakuna popote
katika biblia mwandishi anapata maneno “zaka ya pili”
hata kama anayaangalia makala muhimu katika strong’s
exhaustive concordance. Manano haya ni dawa ya
kujitengenezea inayojaribu bila fanaka kuelezea
kinaganaga maagizo kuhusu zaka katika nyakati za Musa.
Pili, kama andiko hili lingezungumzia zaka ya pili kwa
nini Musa alikuwa anawakumbusha wasomi mara mbili katika
mistari ya 27 na 28 bila kusahau mlawi aliyepokea zaka
ya kwanza. Kwa hivyo kupokea kutoka kwa zaka ya kwanza
mlawi hangehitaji sehemu inayoitwa zaka ya pili.
Kumbukumbu 14 inazungumzia kuhusu zaka ya kwanza na ya
kipekee. Tatu kama makanisa yanaamini udanganyifu wa
zaka ya pili kwa nini wasitengeneze nafasi katika
bahasha za matoleo kwa mhisani kusihi zaka yake itolewe
kama ya kwanza au ya pili. Zaka ya pili inafanya kama
kizuia moshi ambayo matokeo yake ni kuchanganyikiwa wala
sio ufafanuzi.
NI NINI KAPAUMBELE CHA KANISA LAKO?
Sasa wacha tufanye marudio ya haraka kuhusu jinsi kanisa
inayotimiza mahitaji ya wajane, kukiwa na maskwota. Ni
makao mangapi wajane makiwa na maskwota yanayosaidiwa na
kanisa katika kijiji chako? Kama ungejibu hakuna hata
moja kwa moja ya maswali haya kwa nini hayapo?
Kwa upande mwingine ni makanisa mangapi yanayofanya kazi
katika kijiji chako? Mengi bila shaka! Ni viongozi
wangapi wa injili wa kulipwa waliopo pengine asilimia
99.9 yana wahubiri au wazee wa kanisa.
Yawezekana kuwa makanisa mengi ya kikristo hayaendeshi
makao ya makao ya wajane au maskwota vijijini mwetu kwa
sababu ufadhili mkubwa katika makao makuu ya kanisa
unatumika (i) kujenga upya (2) kulipia mishahara, nyumba,
gari za kisasa masomo na nauli za viongozi wa kanisa?
Kama aya tatu zilizotangulia zinazungumzia jamii yako na
kanisa si ni wakati wa kubadili kipaombele cha Mungu
katika kumbukumbu 14 na Matayo 25?
Wakati Waisraeli walipofuata maagizo katika Kumbukumbu
14 – 11 kutimia zaka kusheherekea Baraka ya Mungu kwa
mtoa zaka na familia yake na kudidhia Walawi na mahitaji
mengine mtoe zaka alihakikishiwa baraka za Mungu na
bidii yake.
Je ni nini kipaumbele cha kanisa lako? Tusaidie ulaji wa
kikanisa au mahitaji ya binadamu?
MAFUNDISHO YA MALAKI KUHUSU ZAKA
Kabla kuacha suala la kutoa zaka katika agano la kale,
wacha tusome Malaki kwani ni katika kitabu hiki viongozi
wa kiroho wa kikristo hufundisha uongozi wa kikistro.
Hapana shaka umehudhuria mahubiri juu ya zaka na
ukaambiwa na mhubiri kuwa kama hautalipa zaka kwa kanisa
la mhubiri basi ‘unamwibia’ Mungu. Wacha tusome kitabu
cha Malaki tuone ni kipi mtabiri anasema.
Sura ya kwanza inaanza pale Mungu anapowahakikishia
Waisraeli kuwa anawapenda. Ndipo katika fungu 6 – 8
Mungu anasema “Ni nyinyi wahubiri muonyeshao madharau
kwa jina langu” mhubiri anauliza “Ni vipi tumedharau
jina lako? (NIV), Mungu anajibu munaweka chakula
kilichonajisiwa katika madhabu yangu kwa kuleta wanyama
vipofu, viwete na wagonjwa ‘fungu 9’ anarudia haya
katika fungu 13 Mungu anaonya kuwa hatakubali kafara
hizi duni (New Century Version). Tena katika fungu 14,
Mungu anaona hili.
Katika sura ya pili Mungu anawazungumzia wahubiri
akiwaambia kuwa wamefundisha taifa kutenda mabaya.
Mabaya haya bila shaka yalijumlisha wahubiri kutotilia
mkazo umuhimu wa watu
(1) Kuhakikisha haya mahakamani na (2) Umuhimu wa zaka
na toleo la kafara isiyo chachu kwa Mungu (fungu 7 - 9).
Katika sura ya tatu Mungu anasema kwa nini amekasirika.
Shida ni ipi? Tena wahubiri wanaweka kafara nzuri na
siha huku wakitoa wanyama viwete, vipofu na wagonjwa
kama kafara kwa Mungu na wahitaji walio na sehemu ya
zaka. Mungu anawalaani wahubiri kwani katika sura ya
3:5, anasema, “nitashuhudia tena wale wanaodanganya
wajane na yatima. Na nitashuhudia ya wale wanaowadhulumu
wengine (New Century Version).
Kumbuka kuwa pamoja na walawi, makundi haya matatu ya
wahitaji ndiyo yaliyohidhinishwa kupokea zaka katika
Kumbukumbu la torati, sura ya 14.
Kwa hivyo shida iko na wahubiri walio walafi na
wanaomnyanganya Mungu kafara njema na wahitaji chakula
kizuri kiletwacho kama zaka na wakulima.
Sura ya 3:8 inauliza; “binadamu atamuibia Mungu?”
Wahubiri wanataka kujua walivyomwibia Mungu. Mungu
anajibu “kwa zaka na matoleo”. Kwa sababu hiyo, ghadhabu
ya Mungu ni kupitia kukosana, wahubiri wamejiwekea
yaliyo mema! Wahubiri ni wezi! Sura ya 9 inapendekeza
kuwa sio tu kuwa wahubiri wamemwibia Mungu lakini pia
kuwa wameliibia “taifa nzima” kwa kumfanya Mungu
kukatalia baraka zake kwa watu wake. Kwa kuongezea watu
kuwaona wahubiri wakijiwekea yaliyo bora na kuiga ulaji
wa wahubiri walileta wanyama duni kwa Mungu pia.
Kwa hivyo ni wazi kuwa Mungu hazungumziii swala la
kukatalia zaka na matoleo kabisa anawazungumzia wale
wanaojiwekea wanyama bora badala ya kumtolea Mungu na
kuwapa masikini.
Kwa hivyo Mungu anamzungumzia nani? Anawazungumzia
wahubiri na waliomwibia Mungu na masikini kwa kujiwekea
wanyama bora, (kutilia mkazo ni kwangu) kwa mfano,
wahubiri waliwafundisha watu kuwa walafi. kwa hivyo,
wakati mwingine mhubiri wako akisoma Malachi 3:8 na
kuwanyoshea kidole kumbuka haya ni wazi kuwa mnatakikana
kumnyoshea kidole.
Kiongozi yoyote wa kanisa akiharibu maagizo ya Biblia
kwa kujinufahisha kidole cha lawama ya Mungu hunyooshewa
yeye kwani sio mkusanyiko anaodai kuongoza kwa njia za
Mungu (Malaki 2:8).
SURA YA PILI
FUNDISHO LA AGANO JIPYA
KUHUSU KUTOA ZAKA
Matayo anataja zaka katika sura ya 23:23. Yesu
aliwakashifu viongozi wa wayahudi kwa kutilia mkazo zaka
bora huku wakisahau “maswala muhimu, huruma na uaminifu”.
Wafarasayo ambao Yesu alikuwa akiwazungumzia walikuwa
kwa wakati huu chini ya sheria za Musa, kwani kifo cha
Yesu hakikuzimaliza tu hizi. Tunasoma haya zaidi pale
tunapofuka kwa maandisi ya Paulo.
Tena, hakuna rekodi kuwa Yesu au watumwa walikubali zaka
kwao wenyewe. Tulivyoona katika Kumbukumbu la Torati 14
kutoa zaka lilichukuliwa kuwa nafsi ya mkulima
kusherehekea na kumshukuru Mungu kwa baraka zake,
sherehe ilikuwa kati ya Mungu na mkulima.
Hata hivyo vile agano jipya linavyoandikisha, Yesu na
wafuasi ake walijitolea kwa kuwalinda masikini wenye
njaa, wagonjwa na wahitaji.
Yesu aliwezaje? Akiwa mototo wa seremala? Yawezekana
alifanya kazi kwa mikono yake, tunajua kuwa Yesu
alifadhili kupita kwa kujitolea kutumia zawadi za
marafiki (Luka 8:3) tena Yesu alikubali kupewa na
marafiki, kwani katika Matayo 10 na Luka 10, alituma
watumwa, akiwaambia kuchukua tu nguo walizovaa na kusema
kuwa, “mfanyakazi apewe anachohitaji mshahara wa kila
mara kutoka kwa zaka ya mkusanyiko, wakati tunakubali
zawadi za kujitolea, mtu husema (kama unaweza kunipa
kitu fulani kunisaidia katika kazi yangu ya kikristo, na
kama anahitaji usaidizi, nitaukubali huo usaidizi.
Ingawa kama hunaweza kunisaidia naamini Mungu atanipa.
kwa hivyo kwa wema wa Kristo nitaendelea kukuhudumia!)
Mfano mwafaka wa kutoa na kupokea unapatikana katika
fumbo la Kristo la msamaria mwema Yesu aliwaambia
wafuasi wake waige mfano wa msamaria mwema na wasidai
malipo.
Kitendo kisicho cha watumwa cha kukodi kiongozi wa
kiroho chaonekana kuwa na mizizi yake katika nasaha ya
kikatoliki kuwa lazima kuwe na binadamu mpatanishi kati
ya binadamu na binadamu na huyu awe mhubiri, sio Kristo.
Paulo anasema wazi kuwa kuna mpatanishi mmoja tu , naye
ni Yesu. Kwa bahati wakati waprotestanti walipoondoka
kwa kanisa ya Katoliki walikataa kifungu hiki, kwa
bahati mbaya, hawakukataa kile cha kulipa mishahara kwa
wahubiri. Alexander Campbell anasema vizuri: kuajiri
watu kuhubiri kwa mkusanyiko wa kikristo ni kinaya juu
ya mkusanyiko uliowaajiri ………… ndio yeyote alipwaye
kuhubiri …………… naamini ni utamaduni wa upuniaji, (1830,
imenukuliwa katika ‘Examiner’, Sept. 1993). Hakuna
nakala ya agano jipya ambapo Yesu au watumwa wake
walikubali mishahara na marupurupu kwa kazi yao. Kwani
wao sio mifao yetu? Je, tusaidie ulaji wa kikanisa au
mahitaji ya kibinadamu?
BAADA YA MSALABA
Sasa tutasoma kama ua la zaka inaagizwa baada ya kifo
cha Yesu msalabani.
Wakati Kristo alisulubishwa kitambaa cha hekalu
kiliraruka kuashiria kuwa sheria za Musa zimekwisha,
Paulo alizungumzia jambo hili kwa kusema kuwa mahitaji
ya sherehe kama “nyama” na “vinywaji” siku takatifu na
sabato ya sherehe havikuwa na maana baada ya kifo cha
Kristo, kafara kuu, (Wakolosai 2:16, 17na Waibirania
9:8-11).
Kwa sababu kutoa zaka kulikuwa sehemu ya sheria za Musa
na kwa sababu hili lilimalizwa na kifo cha Kristo si
mahitaji ya zaka yangekataliwa pia? Ndio, kutobadilika
kama vile na (kumbukumbu la torati 12:1-6).
Zaka, tohara na sherehe za kuosha, wanyama kuteketezwa
n.k zilikomeshwa na kusulubishwa kwa Yesu (Wagalatia
5:6; 6:15; na Korinto 7:19).
Kwa sababu Paulo ni mfano wa pili wa Kristo katika Agano
Jipya ni mkristo anayefaa kama mfano na kielelezao kwa
mkristo wa kisasa.
Kwanza hakuna ushahidi wa Biblia kwamba Paulo alikubali
zaka mwenyewe. Anajisifu kwamba ameifanya inchili bure
kwa Wakorinto (1 Wakorinto 9:15) ni mara ngapi umesikia
mhubiri akihubiri zaidi ya fungu la 14? Kwa nini
wanasimamia fungu la 14 inawezakuwa ni kwa sababu Paulo
katika fungu la 15 – 18 anaeleza vile hawezi kukubali
mshahara kwa kazi aifanyayo. Mshahara wa Paulo ni furaha
apatayo kwa kuwahudumia wakristo kwa moyo wake (1
Wakorinto 9:15-27).
Paulo anaandika katika fungu la 8 kuwa aliwaibia kanisa
kwa kuwasaidia kwa kupokea msaada.
Katika kigiriki tunaona kuwa jina kusaidia katika
tafsiri nyingine ni mshahara. Kwa hivyo Paulo alipokea
vyakula vilivyopikwa kutoka kwa marafiki kwa hizani.
Jina kusaidia limetumika kwa sababu zifuatazo: -
(a) Paulo anaelezea vizuri katika Wakorinto wa kwanza
kuwa alipeana injili bila malipo.
(b) Kam alipokea mshahara aliohitaji mbona aliwaambia
Wakorinto kuwa liibia kanisa zingine ili kuwatumikia wao.
Paulo alikubaliana na zawadi na wala si mshahara.
(c) Mambo ya chakula kilichopikwa katika mafundisho ya
Paulo yanaonyesha kukubaliana na zawadi za kujitolea
kama vile Yesu alifanya.
Yeyote atakayehubiri ya kwamba Paulo alihubiri kinyume
atakuwa anajipendekeza mwenyewe wala Paulo hakupokea
zawadi tu bali alifanya kazi kwa mikono kupata riziki? (Matendo
20:34) ni nini la mwisho ulimwona mchungaji wako
akifanya kazi kwa mikono yake kusaidia huduma, (2
Watesolonike 3:6 - 13). Paulo anasema alifanya kazi
usiku na mchana ili asile chakula cha watu bila kulipia
na huu mfano wa kufanya kazi unastahili kwa wote 1
Wakorinto 11:1 “Mnifuate mimi kama mimi ninavyomfuata”.
Paulo ni mfano mzuri wa mkristo mzalishaji mali, mwenye
furaha na kujitolea, kwa kiongozi yeyote wa kiroho
kupata riziki kwa kujitolea bila kuitisha zaka ndio
usimamizi halali.
Kumbuka kwamba baada ya msalaba hakuna ushahidi wa
Biblia kwamba Paulo au wafuazi wa Yesu walipokea wala
kutoa zaka. Paulo anakubaliana na Kristo kuwa
wafanyakazi wa kiroho wapokee vipawa. Matendo 18 – Paulo
anaelezea kuwa waliishi na Aquila ana Priscila wakifanya
kazi ya kushona hema. Pia walikutana na Yusto mcha Mungu
akamkaribisha.
Hakuna mahali katika Biblia ambapo Paulo au Yesu
alifundisha kuwa wahubiri wapokee mishahara. Je tuunge
ulaji wa kikanisa au ulaji wa kibinadamu?
Yatarajie mengi.
SURA YA TATU
KUTOA KWA MAKUANI WAKUU
Tumeona kwamba mtindo wa sherehe katika agano la kale
ulimalizwa wakati Yesu alifuka kwa ajili ya dhambi zenu.
Yaliokataliwa na mtindo huo ni pamoja na: - makuani wa
kwanza, tohara, zaka, wanyama kuteketezwa na sherehe za
kufua n.k.
Katika kujitolea kwake Yesu Myaudi alifanyika kuani mkuu,
Waeberania 7, Paulo anaonyesha kuwa makuani wa kwanza
walikufa na badala yao makuani wengine wakachukua
usukani. Melizedeki mkuu wa amani (fungu 2) na uzima (ambaye
Abraham alipeana zaka kwake) ni kioo cha kuani mkuu
Messiah Kristo aliye na uzima. (Fungu la 5) inasema kuwa
Mlawi aliyefanywa kuani angepewa amri ya sheria za
shelee kupokea fungu la kumi la nyongeza ya mkulima.
Ingawaje tumeona sheria za sherehe zilikomeshwa na kufa
kwa Yesu, hakuna mchungaji ambaye atajiondoa kwa wenye
dhambi kama yeye si mtakatifu. Weabrania 8:1 na 6
inamtoa Yesu kama kuani aketiye kitini cha enzi
akihudumu kama mpatanishi mkuu.
Biblia inasema wazi jinsi ya kumpatia kuani wetu Mathayo
25:34 Kristo anasema atatawanya kondoo na mbuzi,
watakatifu kutoka kwa wabaya, kondoo atawakaribisha
mkono wake wa kulia katika ufalme. Ndiposa Mungu
atawaelezea kwa nini atawakubali waliokoka; nilikuwa na
njaa mkanilisha, nilikuwa na kiu mkanipa maji, nilikuwa
bila makao mkanipa, nilikuwa uchi mkanifisha, nilifungwa
mkaja kuniona.
Ndiposa watakatifu watauliza “Ni lini tulikutendea
haya?”(fungu 40) Ikiwa umemmfanyia mwenzako umenifanyia
mimi. Je ni njia gani tunampa kuani mkuu? Ni kwa
kuwasaidia ndugu na dada zetu wenye mahitaji.
Kwa hivyo hatumpi yesu kwa kutuma zaka zetu kwa maofisi
ya kanisa ambapo hupokelewa na wasio walawi na kutumia
kama mishahara yao na ujenzi.
Angalia kusaidia walio na mahitaji kwa kutoa chini ya
mapato yako katika mpangilio wa walawi wa zaka unaweza
kuwa juu ya mapato yako.
Wakati wa Musa, lilikuwa utawala wakati watu walitoa kwa
kanisa walito utawala. Leo hii kanisa ni tofauti na
utawala. Katika Amerika. Asilimia 45% uenda kwa utawala
kwa kanisa zaka ni 10% na asilimia 0.5% inaenda kwa
wasiojiweza makao ya myatima wanapeana 60% kwa manyumba
yao. Ni wazi kwamba asilimia 40% ya mapato yalibakia
wafanyikazi, walawi katika wakati wa Musa walikuwa
60-70% ya mapato yao hubakia kwa matumizi yao. Wakristo
wengi hawako macho kama vile kwa siasa.
Siku hizi baada ya Yesu kutukomboa tunapeana kwa kuwani
Mkuu kwa kuwalinda wenye mahitaji. Je kanisa lako
linatilia maanani kusaidia wenye mahitaji au ni kununua
mashamba kujenga nyumba. Kuna viongozi wa kanisa
wanaosema kwamba.
Kujenga manyumba mapya kunaonyesha “kukua kiroho”
Hakuna mahali yesu amelinganisha ujenzi wa kanisa na
ukuaji kiroho. Anasema analinganisha ukuaji kiroho kwa
makadilio ya sisi kulinda wajane, yatima, walio na kiu,
wasio na makao na walio njaa.
Kutumia makadilio ya Yesu kanisa lenu limefanya mazuri
kufika wapi? Je tuunge ulaji wa kanisa au alaji wa dini?
(Yatarajie mengi)
SURA YA NNE
NAFASI YA MADALIKO KANISANI
Kulingana na ushahidi ulijitokeza juu ni kwamba bado
kanisa zingine zachukulia sheria za sherehe za kutoa
zaka ya fungu la kumi kila mwaka kwa lazima> Ingawaje
hii ni nafasi ya ufalisayo na tunaangalia juu yake
tutilie maanani kidogo:
Kama kweli sheria za sherehe hizi bado zafuatiliwa mbona
kanisa zingine hazifuatilii mambo yanayolingana na
sherehe kama:-
1. Makuani wa walawi hawakuruhusiwa kurithi shamba. Hizi
kanisa huwazuia wahubiru kurithi mali?
2. Kumbukumbu la torati 14, lasema kuwa fungu la kumi
liende malango ya mkulima ili yalishe yatima wajane
wageni pamoja naye mkulima na familia yake.
Je umewahi kusikia muhubiri akisema kuwa kutumia fungu
la kumi waumini mulisha familia zenu?
3. Hawali katika siku za malaki makuani waliokuwa na
tamaa walijichukulia mazao mazuri kwanza na kupeana
mazalio kwa Mungu na amskini. Bado Mungu siku hizi
huwalaani wachungaji wanaojipatia mshahara mzuri ilhari
wanaosumbuka kwa jamii bila mahitaji ya kimsingi wapo?
4. Kikristo kulingana na kazi ya wachungaji wa sasa
makuani wakati wa Musa ni ufalisayo mtupu. Makuani wa
agano la kale walitoa sadaka ya keteketezwa na kuwa
wapatanishi kati ya Mungu na wanadamu. Siku hizi
wachungaji huwahudumu kama wapatanishi wala kutoa sadaka.
Kristo pekee ndiye mpatanishi wa uzima aliyeketi mkono
wa kulia wa Mungu aliyejitolea kufa msalabani kwa ajili
ya dhambi zetu.
5. Ni makuani wa walawi pekee waliostahili zaka
mchungaji wako ni wa kabila la walawi?(Hesabu 3)
6. Kanisa lafunza kuwa kila mapato yatolewe katika fungu
la kumi lakini walawi 27 yasema kuwa ni mapato ya shamba
na matunda ya miti yangetolewa zaka. Amri hii iliwaweka
nje waashi wavuvi,wanaoshona nguo, viatu na mikeka n.k.
Ni bayana kuwa mkristo wa kawaida kanisani anatengeneza
pesa kuliko kuhubiri ukweli neno la Mungu.
7. Walawi walitakiwa kuleta zaka yao ya chakula wala si
pesa. Kama wangeleta pesa walikuwa wanatoa asilimia
ishirini 20% juu yake- walawi 27:30. Vile tumeona
wakristo wa kisasa hawaja acha kufuatilia sheria za
sherehe mzima. Kanisa lataka waumini kufuata kipande
kimoja kinachowaezesha kuwa tajiri na kupokea mishahara
mizuri. Je tuunge mkono tamaa ya makanisa au tamaa ya
wanadamu?
SURA YA TANO
MIFANO YA UKWELI KATIKA MAISHA
Ilikuwa mwezi wanne na jua kali mhubiri Smith
(protestant) alikuwa akiendesha gari na nduguye Brown
mkuu wa Deacon mbele ya masaa matatu kanisani ya mkutano
wakawa wanacheza mpira wa golf huu mkutano ungekuwa wa
maana na mada kuu zilikuwa; (1) jinsi ya kupata pesa za
kuongeza kanisa mpya iliyoko Riverside Drive.
(2)Kumuadhibu Deacon wa kanisa, huyu Deacon alikuwa
akitumia pesa za kanisa kwenda kwa yatima wa salvation
army badala ya kutumia pesa kanisani zifanye mipango ya
kanisa. Haya ndiyo yaliyokuwa mashtaka yake.
Kama wanaendelea kucheza simu yake mhubiri Smith ikali.
”Hello” alisikia mwanamke kutoka upande mwingine wa simu
akisema hana makao anasafiri kwenda Baltimore kutoka
Charlotte ambako watakaa na mototo wake wa miaka mitatu
hadi apate kazi.Gari lake la aina la 1981 Honda ya huyu
mwanamke lilikuwa linahitaji pauni 38 zilizobaki
kutengeza radiator ambayo ilikuwa inatakiwa pauni 74.39
Aliangaika na kushindwa kama mchungaji huyu atampa
usaidizi wa kupata radiator nyingine kwa kumuongezea
pesa anunue mpya.
Mhubiri kumjibu alimwambia ya kwamba yu garini akisafiri
kwenda mkutano na Deacon mkuu hangeweza kumsaidia
ampigie simu keshowe atapata wakati wa kuongea naye aone
kama katika matumizi ya kanisa kungepatikana na pesa za
kukomboa nyumba. Hata hivyo alimshukuru kwa muda aliompa.
Huyu mwanamke aliangalia upande mwingine na kuona
mwanamke wa salvation Army volunteer aliyekuwa
akitengeneza gari yake. Alimweleza shida yake akakubali
kumsaidia kumtengenezea gari lake kwa garage. Kumchukua
na mototo wake awape chaakula na mahali pa mapumziko
ndiposa waendelee na safari yao ikiwa vizuri.
Kati ya hawa wakristo ni nani atapata Baraka za Mungu
akirudi kuwatawanya kondoo na mbuzi. Ni shirika lipi
latoa kwa kristo aliye kuani mkuu? Kulingana na hadithi
hii ni mhubiri Smithh au ni kijana wa Salvaton Army?
Tuunge tama ya makanisa au tamaa ya ubinadamu?
MARUDIO KATIKA NJIA YA MUHTASARI
Tumejifunza kutoka kwa bibilia kuwa :-
a) Zaka ilihitajika kulingana na sheria za walawi
b) Zaka, fungu la kumi ilikuwa nyongeza ya mapato ya mtu
c) Zaka ilitumika kusheherekea Mungu vile vile kusaidia
walawi waliokuwa wajane yatima na wasio na makao.
d) Wakati mwingine makuani walipuuza zaka kwa kujiwekea
vinono na kutojali wanyonge/ maskini.
e) Baada ya kusulubiwa na kufa kwa Yesu msalabani kwa
ajili ya dhambi zetu sherehe za kisheria ikiwepo tohara
na zaka ziliwekwa kwa lazima kila mwaka.
f) Paulo, watumwa na Kristo mwenyewe alikubaliana na
kupewa zawadi kutoka kwa marafiki.
g) Katika bibilia hakuna mahali tunaona kuwa Paulo,
watumwa na kristo walipokea zaka wala kutoa wala
kutegemea zaka kwa kuwalisha.
h) Mtindo wa sherehe wa makuani kutoa sadaka kuteketezwa
ulimalizwa na kuani mkuu aketiye kitini cha enzi
akihudumu kama mpatanishi mkuu kati yetu sisi na Mungu.
i) Yesu anatwambia kuwa ikiwa twataka kuhesabiwa wenye
haki arudipo mara ya pili lazima tuwahudimie maskini
wasio na makao na waliofungwa
Kwa baati mbaya wakristo kanisani wameamua
1. Kupuuza mafundisho ya Paulo
2. Kuwalipa wachungaji mishahara mikubwa kutokana na
pesa za waliokufa.
3. kutofanya kazi hili wajisaidiea wasiojiweza kama
Kristo na Paulo ambao wanatumika kama mifano mizuri
katika kanisa la leo.
Tabia ya kutoa zaka na sheria za sherehe, kanisa
kukubaliana mambo haya sherehe zilizokufa na kwa kufanya
hivyo wanakataa damu ya Yesu mkombozi na mpatanishi wetu.
Kwa wasimamizi wa kanisa kupuusilia mafundisho ya
bibilia ni tendo ambalo haliwezi kuepukika na wasimamizi
wanaodai kuwa wanaelekeza wafuasi wao kwa njia ya kweli
kulingana na mafundisho ya bibilia.
Ikiwa unatoa zaka au kupokea zaka utafanya nini na kwel?
Jibu lako kwa swali hili bila shaka litakuwa na matokeo
ya uzima!
Mungu akupe nguvu ya kusimama na ukweli vile
unaejitahidi kulisha kondoo, kufuata neno lake na
uhesabiwa katika watoto wake katika kurudi kwake mara ya
pili.
MFANO WA KUMALIZIA
Si kitambo sana mchungaji an kristo walikuwa wanatembea
kijijini cha mtaa mmoja. Katika mlango wa nyumba
iliyoamwa kulikuwa na kijana wa miaka saba aliyevaa nguo
chafu kijana aliwaangalia Yesu na mchungaji. Alikuwa na
nywele ndefu, chafu nguo zilizoraruka na viatu
vilivyoisha na miguu kutokea nje. Mchungaji alimuuliza
Yesu mbona unaharibu wakati kwa mtu asiyefaa? Yesu
alimwangalia mchungaji na kumjibu “Ni mimi niliyekuumba
wewe na ni mimi niliye muumba huyu ndugu”
SWALI LA MWISHO
Je wewe na kanisa lako mtaendelea kuhesabu ufanishi kwa
kuongezeka kwa watu kanisani, nyumba, nyongeza ya zaka
mishahara ya utumizi au wewe na kanisa mtatoa mliconacho
kwa chokora?
Kumbuka ni Yesu aliyemwita chokora nduguye! Utafanya
nini na nduguyo mkombozi wako?
Utafanya nini na huyo mototo? Mwishowe, Utafanya nini na
kristo?
Kwa mengi zaidi wasiliana na :-
Daktari Fillimer Hevener
(434) 392-6255
E-mail
COPYRIGHTED 2001,
BY FILLMER HEVENER
224 MOHELE ROAD
FARMVILLE, VIRGINIA 23901
(434) 392-6255)
(All rights Reserved. No portion of this document may be
reproduced in any way without the written consent of
Fillmer Hevener. Please email him for written
permission to reproduce this article.)
|